Rico, Suzuki: Malumbano baina ya wazazi yalaza ndoto ya biashara

Posted on June 16, 2010

2Wasanii Rico na Suzuki wanafahamika vyema kwa mistari laini na kufana kwao katika mziki huu wa kizazi kipya.

Rico Na Suzuki, licha ya kwamba ni marafiki wa dhati, sasa wanajipata katika njia panda baada ya ndoto yao ya kujiendeleza kibiashara kukumbwa na misukosuko, kutokana na kutoelewana kwa mama zao.

Mapema mwaka jana, Rico na Suzuki walifungua hoteli ya maankuli katika eneo la Bamburi, kwenye barabara inayoingia Lakeview.

Walikodi maduka mawili na kuanzisha biashara hiyo huku wakiwaweka wazazi wao kama wasimamizi….jambo ambalo limebainika sasa kuwa kosa kubwa.

Baada ya wiki chache, malumbano yaliibuka huku Mamake Rico na Suzuki wakijamishana “Laivu laivu” hadharani, na kupelekea kudidimia kwa biashara.

Mdokezi wetu anatufahamisha kwamba kwa sasa biashara hiyo imeanguka huku wakilazimika kurejesha mlango mmoja wa duka kwa mwenyewe na kubakia na mmoja…..

Suzuki akifanya vitu vyake

Mamake Rico amejiondoa katika mradi huo.

Letu ni jicho tu.