YOU MUST SEE THIS!!! Only In Bongo~!

Posted on March 30, 2012

2Huyu bila shaka ndiye msanii mkongwe zaidi wa Bongo Flava.

Anaitwa Bibi Cheka!!!

The oldest Bongo Flava Artiste in Tanzania..Bibi Cheka

MSANII wa muziki wa bongo fleva, kutoka kundi la Wanaume Family, Mh Temba, amefurahishwa na kujitosa ukumbini kwa msanii mpya waliyemsaini ndani ya lebo yao anayejulikana kwa jina la Bibi Cheka. Tayari wametoa video collabo na msanii huyo wimbo ukijulikana kwa jina la ‘Ni wewe’. VIDEO IKO HAPA CHINI.

Temba alisema msanii huyo jina lake limeendana na umri wake kwani ni mtu mzima ingawa anafanya muziki mzuri kuliko hata wasanii wachanga na wabana pua.

Alisema kuwa wamemchukua bibi huyo kutokana na uwezo wake wa kuimba hivyo wanaamini wimbo huo utaweza kumtambulisha ndani ya game.

“Tupo katika mchakato wa kupiga picha za video ya wimbo, ambao ni wa msanii wetu mpya tuyeliyemsaini ndani ya lebo yetu, hivyo baada kazi yake kumalizika tutakuwa katika mchakato wetu kama kawaida,” alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa kwa upande wake atatoa wimbo mpya mwanzoni mwa mwezi Aprili kwani sasa anafanya mchakato wa kumtambulisha msanii huyo.

“Kwa upande wangu sina wimbo wowote ambao naweza kusema kwamba utakuja hivi karibuni, kikubwa ni kwamba hadi April hapo ndo kazi zangu mpya zitaanza kusikika,” alisema Temba.

Tazama Video hiyo hapa:

Posted in: Entertainment